Uteuzi na mabadiliko Wakuu wa Wilaya

RAIS, Samia Suluhu Hassan Amemteua Elibariki Bajuta, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa
Uhifadhi, Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro kuwa Mkuu wa Wilaya ya Urambo.

Bajuta anachukua nafasi ya Kenan Laban Kihongosi ambaye amehamishiwa Momba.

Aidha Rais, Samia Suluhu Hassan Amemteua William Simon Mwakilema, Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kuwa Mkuu wa Wilaya ya Korogwe.

Advertisement

Mwakilema anachukua nafasi ya Jokate Mwegelo ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT).

Katika hatua nyingine, Rais Samia  Amemhamisha kituo cha kazi Mkuu wa Wilaya ya Urambo, Kenan Laban Kihongosi kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Momba Mkoani Songwe.

Kihongosi anachukua nafasi ya Fakii Raphael Lulandala ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa UVCCM.

Rais,Samia pia  Amemhamisha kituo cha kazi Sixtus Raphael Mapunda kutoka Wilaya
ya Sumbawanga kuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke.

Mapunda anachukua nafasi ya Mobhare Holmes Matinyi ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari –Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali.

4 comments

Comments are closed.