Utitiri wa mashauri mahakamani wapungua

KATIKA kupunguza mlundikano wa mashauri mahakamani, jumla ya mashauri 252, 882 yaliwasilishwa katika kipindi cha mwezi Julai 2023 hadi Ma hi 2023 ambapo  kati ya hayo mashauri 199,122 yalisikilizwa na kuhitimishwa.

Waziri wa Sheria na Katiba, Damas Ndumbaro akiwasilisha bajeti ya Wizara yake Bungeni mjini Dodoma leo Aprili 25,2023 amesema mashauri 53,760 yanaendelea kusikilizwa.

Ndumbaro amesema  mashauri  2,414 ni ya mlundikano, sawa na asilimia 4 ya  mashauri hayo yaliyopo Mahakamani.

Advertisement

Aidha, amesema kati ya mashauri 252, 882 mashauri 58,266 ni yaliyokuwepo mwanzoni mwa mwezi wa Julai 2022