Uturuki, Somalia kushirikiana kwenye mafuta, gesi

UTURUKI imesaini mkataba wa ushirikiano wa mafuta na gesi asilia baharini na Somalia , Wizara ya Nishati ya Uturuki ilisema.

Hatua hiyo ni katika kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizo mbili baada ya makubaliano ya ulinzi mwezi uliopita.

Wizara ya nishati ilisema makubaliano hayo ambayo iliyataja kama makubaliano ya kiserikali, yanajumuisha uchunguzi, tathmini, maendeleo na uzalishaji wa mafuta katika bahari ya Somalia.

“Kwa makubaliano haya, tutafanya shughuli za pamoja za kuleta rasilimali za Somalia kwa watu wa Somalia. Tunalenga kuimarisha uwepo wa Uturuki katika Pembe ya Afrika kwa ushirikiano mpya katika uwanja wa nishati,” Waziri wa Nishati Alparslan Bayraktar alisema.

“Utafiti wa mafuta na gesi asilia katika Pwani ya Somalia, na inaonekana zaidi kama mafuta kwa sasa, utaanza hivi karibuni katika maeneo ambayo tumeyatambua”

Habari Zifananazo

Back to top button