Uturuki yarusha makombora Iraq

VIKOSI vya Uturuki vimefanya mashambulizi mapya ya anga Kaskazini mwa Iraq na kuharibu maeneo lengwa 16 ya chama kilichopigwa marufuku cha Wafanyakazi wa Kurdistan (PKK), Wizara ya Ulinzi imesema.

Al-Jazeera imeripoti kuwa operesheni hizo zilifanyika katika mikoa ya Metina, Gara, Hakurk, Qandil na Asos saa nane mchana (17:00 GMT) Jana Jumanne, wizara hiyo ilisema na kuongeza kuwa kila hatua ilichukuliwa ili kuepusha madhara kwa raia.

Imeelezwa kulikuwa na mlipuko wa bomu mbele ya majengo ya Serikali ya Uturuki mjini Ankara siku ya Jumapili na kukatisha maisha ya watu wawili pamoja na kujeruhi maafisa wawili wa polisi.

Aidha kwa mujibu wa Al-Jazeera kundi la PKK, lililoorodheshwa kama “kundi la kigaidi” na Uturuki na washirika wake wa Magharibi, limekuwa likiendesha mashambulizi tangu 1984 na kuua maelfu ya watu.

Msururu wa operesheni za kijeshi za Uturuki zimerudisha nyuma kundi hilo katika nchi jirani ya Iraq.

Habari Zifananazo

6 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button