UVCCM Songwe yatia neno mikopo ya vijana

MWENYEKITI wa Umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Mkoa wa Songwe,Fatuma Hussein amewatoa hofu vijana kutokana na serikali kusitisha utoaji wa mikopo ya asilimia 10,iliyokuwa inatolewa na halmashauri nchini na kusema mpango bora zaidi wa utoaji frdha hizo unaandaliwa.

Ameyasema hayo katika ziara ya kamati ya utekelezaji ya UVCCM Mkoa wa Songwe ambayo inatembelea wilaya mbalimbali za mkoa huo.

Fatuma amesema UVCCM wanaamini kuwa serikali itakuja na mpango bora zaidi wa utoaji wa mikopo hivyo kuvitaka vikundi ambavyo vilikwisha undwa kuendelea kujiandaa na pindi dirisha la mikopo litakapozinduliwa wawe wa kwanza kunufaika na fedha hizo.

Advertisement

Aidha katika hatua nyingine Fatuma ameiomba serikali kuharikisha ujenzi wa Soko la Tunduma linalosubiriwa kwa hamu na wananchi ambao wamesema litakuwa mkombozi wa vijana wengi kujiajiri.