Uwanja mpya Dodoma watengewa Sh Bil 55
DODOMA; WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa Na Michezo, Dk. Damas Ndumbaro amesema Serikali inatarajia kuanza Ujenzi wa uwanja cha michezo Mkoa wa Dodoma mwaka 2024/25, ambapo bajeti ya kuanza ujenzi huo jumla ya Sh. Bilioni 55 imetengwa.
Amesema Kiwanja hicho kikikamilika kitakuwa na uwezo wa kuchukua watazamaji 30,000 wakiwa wamekaa.
Waziri Ndumbaro amesema hayo wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa mwaka wa Fedha 2024/25 bungeni jijini Dodoma leo Mei 23, 2024