Uwanja mpya Geita kuwekwa nyasi bandia

Uwanja mpya Geita kuwekwa nyasi bandia

HALMASHAURI ya mji wa Geita imeweka wazi kuwa inatazamia kufanyia mabadiliko uwanja wake mpya na kuondoa nyasi za asili zilizopandwa, ili kuweka nyasi bandia.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Geita, Costantine Moradi ametoa taarifa hiyo katika mkutano Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Geita (GEREFA).

Morandi amesema hadi sasa ujenzi wa uwanja unaendelea na nyasi za asili zilishapandwa, lakini ukaguzi wa mhandisi mshauri umebaini kuna mabonde chini ya nyasi.

Advertisement

“Kwa hiyo tumekubaliana hivyo, yule mtaalamu wa TFF (Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania) aliyekuja, tumempa maelekezo atueleze gharama za kuweka nyasi bandia, tena zile za kiwango cha juu.

“Alitueleza kuna nyasi za viwango vitatu, kwa maana ya A, B na C, na sisi tumemwambia tunataka zile nyasi zenye ubora wa daraja A kama zilizopo chamazi.

 

“Tupo tayari kuhakikisha mkoa huu wa Geita unazidi kukua kisoka, na unakuwa na miundombinu mizuri, baada ya hapo tukishafanikiwa tutaweka taa,” amesema.

Mwenyekiti wa GEREFA, Salum Kulunge ameishukuru halmashauri ya mji wa Geita kwa juhudi za kuendeleza sekta ya michezo na kuziomba halmashauri zingine kuiga mfano huu.

Amesema iwapo uwanja utakamilika kwa wakati, TFF imeahidi kuleta mchezo wa nusus fainali wa kombe la FA kuja kuchezwa mjini Geita.

Januari 2023, Makamu wa Rais wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGML), Simon Shayo alieleza ujenzi wa uwanja huo umefikia asilimia 80 na unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Mei 2023.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *