Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi wafungiwa

UWANJA wa Ali Hassan Mwinyi uliopo mkoani Tabora umefungiwa kutumika kwa mchezo wowote wa Ligi Kuu mpaka pale utakaporekebishwa eneo la kuchezea, Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) limeeleza.

Taarifa iliyotolewa leo na shirikisho hilo imeeleza kuufungia uwanja huo mpaka pale utakapokaguliwa na kujiridhisha kufanyika kwa marekebisho hayo.

TFF imesema uwanja huo umekosa vigezo vya kikanuni na sheria za soka hivyo kwa sasa hauwezi kutumika.

Hatua hiyo itailazimu timu ya Tabora United kutafuta uwanja mwingine kwa michezo ya nyumbani hadi pale uwanja huo utakaporekebishwa.

Aidha, TFF imezikumbusha timu zote kuendelea kutunza na kuboresha miundombinu ya viwanja kwa klabu ambazo hazimiliki viwanja.

Habari Zifananazo

Back to top button