Uwanja wa ndege Dom kufungwa taa

safari za usiku kuanza Novemba

MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la ndege Tanzania (ATCL) Mhandisi Ladislaus Matindi amesema ndege zitaanza safari za usiku katika uwanja wa Dodoma ambao kwa sasa zoezi la ufungaji taa linaendelea na linatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Novemba mwaka huu.

Matindi, ametoa taarifa hiyo leo Julai 02, 2023 katika ziara yake kwenye Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba 2023, barabara ya Kilwa, Dar es Salaam.

“Tunaambiwa kufikia mwezi wa 11 watakuwa wamemaliza na hivyo kuwapa wigo mpana zaidi wateja wanaoingia na kutoka makao makuu ya nchi kuchagua saa ngapi wasafiri.”

Aidha, Matindi amesema kufikia mwishoni mwa mwezi wa saba nguvu yao ya utoaji huduma itakuwa imeongezeka zaidi kwa kuwa kuna uhitaji mkubwa

Akitolea mfano wa Mkoa wa Mwanza Matindi amesema sasa hivi kuna ndege tatu za kwenda Mwanza lakini mahitaji ya Mkoa huo ni zaidi ya ndege tatu

“Tumeendelea kuongeza idadi ya ndege, kwa sasa tuna ndege 12 tegemea kupata ndege tatu zaidi, mbili za masafa ya kati aina ya Boeing 737 na Dreamliner moja.”

Hata hivyo amesema changamoto iliyoikumba ATCL na dunia juu ya ndege za Airbus tayari zimashatatuliwa

Habari Zifananazo

Back to top button