UWT wapongeza kuruhusiwa mikutano ya siasa

Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT),  umesema kuwa uamuzi wa kuruhusu mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa uliochukuliwa na Rais Dk Samia Suluhu Hassan ni mwelekeo mpya wa nchi katika kuihami demokasria.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa UWT Taifa,  Marry Chatanda, wakati mkutano wake na waandishi wa habari mkoani Tanga kutoa salamu za pongezi kwa Rais Samia zinazotokana na matokeo ya mkutano baina ya Rais Samia na viongozi wa vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu uliofanyika jana.

Alisema kuwa uamuzi wa kuondoa zuio hilo ni katika falsafa ya Rais  Dk Samia kujenga upya nchi yenye umoja katika ujenzi wa Taifa, inaongozwa na falsafa yake ya maridhiano, ustahamilivu, mabadiliko na kujenga upya nchi.

Alisema kuwa maridhiano hayo yanaenda kuleta matumaini mapya katika kujenga misingi imara ya demokrasia, yenye umoja kwenye nyanja za kisiasa.

“Kilio chetu UWT siku zote ni kuona nchi yetu ikiwa na utulivu, amani na yenye haki baina ya wananchi wake na serikali yao.

“Rais Samia amechonga palio, wajibu wetu sote wanasiasa na wananchi wote ni kulifuata kwa unyenyekevu hilo palio, tusimkatishe tamaa. Si vijana, akina mama wala wazee, sote tuwe wamoja tujenge nchi yetu,”alisema Chatanda.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x