UWT yapongeza ujenzi shule ya wasichana

MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mary Chatanda amepongeza mradi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Shinyanga ambayo imejengwa kwa gharama ya sh Bilioni 4 .

Kwa sasa shule hiyo inafanya kazi na wanafunzi wanasoma katika mazingira yaliyo salama .

Akizungumza leo katika Ukaguzi wa Shule hiyo ya Wasichana, Chatanda amesema lengo la serikali ya Rais Samia ni kuhakikisha watoto wa Tanzania wanasoma katika mazingira mazuri na Salama ili kuongeza ufaulu mzuri na ndio maana kila Mkoa shule za Wasichana Maalumu zimejengwa .

” Niwaombe watoto wangu kuendelea kutunza Miundombinu iliyopo katika shule yenu kwa kuwa Serikali yenu imetumia fedha nyingi katika kuhakikisha inajengwa shule yenye Miundombinu mizuri na yenye tija kwa wanafunzi katika kuongeza ufauru mzuri ”

 

Habari Zifananazo

Back to top button