Uzalishaji mkonge waongezeka

Uzalishaji wa zao la mkonge nchini umeongeza kutoka tani 36,000 mwaka 2020 hadi kufikia tani 68,000 kutokana na uhamasishaji mkubwa uliofanywa na serikali.

Hayo yamesemwa na Katibu  Mkuu Wizara ya Kilimo, Gerald Mweli wakati wa ziara yake ya siku moja ya kutembelea mashamba ya mkonge pamoja na  Bodi ya Mkonge nchini.

Amesema tangu serikali imeanza kuweka msisitizo kwenye kilimo cha mkonge, uzalishaji wake umeanza kuongezeka kutoka tani moja kwa hekari hadi kufikia tani 2, huku  malengo ni kufikia tani 5 ifikapo mwaka 2025.

Amesema ili kufikia malengo hayo wamewekeana mikakati na Bodi ya Mkonge kuhakikisha kwamba tija inaongezeka kwenye uzalishaji kwa hekari kwa kuimarisha huduma za ugani kwa wakulima na kuiwezesha bodi yenyewe kuwa na vitendea kazi ambavyo vitarahisisha ufanyaji kazi.

Katibu  Mkuu Wizara ya Kilimo, Gerald Mweli

“Ili kumaliza changamoto ya uchakati wa mkonge, serikali imetoa S Bil 1.5 kwa Bodi ya Mkonge kwa ajili ya kununua mashine za korona na kuziweka katika maeneo ambayo yana uhaba, ili kuongeza uzalishaji, “amesema Katibu huyo.

Naye  Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Mkonge Tanzania, Saad Kambona amesema bodi hiyo imeshaanza kutekeleza mikakati mbalimbali ya kuendeleza kilimo cha zao hilo yanayolenga kufikia uzalishaji wa tani 120.000 ifikapo mwaka 2025.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x