Uzalishaji samaki waongezeka Zanzibar

ZANZIBAR: WIZARA ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi inaendelea kuwezesha wajasiriamali na wananchi kwa kuwapatia elimu, uelewa na ufahamu katika ajenda ya uchumi wa buluu.

Uwezeshaji huo ni sehemu ya utakelezaji wa ahadi za Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Ally Mwinyi alizotoa wakati wa kampeni ikiwa ni miongoni mwa mikakati ya kuimarisha uchumi.

Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi, Suleiman Masoud Makame amebainisha hayo katika kikao na waandishi wa habari cha kuzungumzia maendeleo na mafanikio ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar kuhusu uchumi wa buluu na uvuvi Desemba 27, 2023.

Advertisement

Aidha Makame amesema tangu Serikali awamu ya nane iiingie madarakani uzalishaji wa samaki Zanzibar ilikuwa tani 38,107 wenye thamani ya Sh bilioni 205.4 kutoka mwaka 2020, ambapo kwa mwaka kufikia 2023 uzalishaji wa samaki umepanda na kufikia tani 80,000 wenye thamani ya Sh bilioni 569.

Vilevile alitoa ufafanuzi juu ya upandaji wa bei ya mazao ya baharini husababishwa na soko la dunia kama ilivyo kwenye zao la karafuu.

Hata hivyo Makame aliwasihi wafugaji hususani wa viumbe wa baharini kufata taratibu maalum wa kuzingatia maelekezo wanayopatiwa na wataalamu.