IMEELEZWA golikipa wa zamani wa Manchester United, Edwin Van Der Sar amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) baada ya kupata kuumia kichwani na damu kuvuja katika ubongo.
Mholanzi huyo amekutana na changamoto hiyo alipokuwa kwenye mapumziko huko Split nchini Croatia.
Baada ya kukutana na shida hiyo, Van Der Sar mwenye umri wa miaka 52 aliwahishwa hospitali.
Taarifa zaidi kukujia.