Van der Sar apelekwa Uholanzi, abaki ICU

KIPA wa zamani wa Manchester United, Edwin Van der Sar amepelekwa nchini kwao Uholanzi akiwa bado kwenye chumba cha wagonjwa mahututi kufuatiwa kuvuja damu kwenye ubongo wiki iliyopita akiwa Croatia.

Mke wake Annnemarie Van Kesteren ameeleza.

Kipa huyo ,52, ambaye pia amewahi kuitumikia Ajax amekuwa hospitalini nchini Croatia kwa wiki moja ambako alienda likizo.

Katika taarifa iliyotolea na Ajax, mke wake amesema Edwid amepelekwa nchini humo jana Ijumaa.

“Hali yake iko vile vile: tulivu, katika hali isiyotishia maisha,” alisema.

“Familia ya Van der Sar ingependa kutoa shukrani zao za dhati kwa Hospitali ya Chuo Kikuu cha Split kwa huduma yao kubwa wiki iliyopita.”
“Edwin anatakiwa kubaki chumba cha wagonjwa mahututi ambako atachunguzwa zaidi.” Ameongeza.

Habari Zifananazo

5 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button