VAR kufungwa kwa Mkapa

HUENDA sasa waamuzi wa Ligi Kuu Bara wakashusha pumzi kutokana na makosa ambayo wamekuwa wakiyafanya kwenye baadhi ya michezo, baada ya taarifa nje za ujio wa teknolojia ya usaidizi wa video kwa waamuzi (VAR).

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini, Wallace Karia ametoa taarifa hizo njema leo Desemba 16, 2023 katika mkutano mkuu wa shirikisho hilo unaoendelea Iringa.

Karia amefafanua kuwa ufungwaji wa vifaa hivyo utafanywa katika viwanja vinavyokidhi vigezo vya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Ulimwenguni (FIFA).

Advertisement

“Tumepata VAR ambayo itakuwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa” maneno ya Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia.

1 comments

Comments are closed.