Veta Dodoma wabuni mfumo kudhibiti madereva kusinzia

MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo Stadi (VETA-Dodoma) imebuni mfumo wa kudhibiti madereva wanaosinzia wakiwa barabarani lengo ni kupunguza Ajali zinazosababishwa na Uzembe.

Akizungumza na HabariLeo katika Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara ‘Sabasaba 2023’ yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es salaam leo Julai 9, 2023, mmoja wa wanafunzi waliobuni mfumo huo, Paschal Massay amesema siku zote walimu wa chuoni hapo wamekuwa wakisisitiza wanafunzi kutumia elimu yao kutatua changamoto ndani ya jamii

Paschal , amesema ubunifu huo utatatua wimbi hilo la ajali hasa kwa magari ya mabasi  na malori yaendayo mikoani na nchi Jirani i wanaosinzia.

“Madereva wengi wanasafiri umbali mrefu, ili kudhibiti ajali zinazotokana na usingizi, tumetengeneza miwani ya kielektroniki ambayo itakuwa inampa taarifa dereva kuwa anasinzia kwa hiyo tumeweka vitu vya kielektroniki kwenye mfumo ambavyo vinahesabu mikonyezo,” amesema na kuongeza

“Mwanadamu ambaye ni mzima anakuwa na mikonyezo ya macho (kufumba na kufumbua) mara 15 hadi 25 kwa dakika moja. Mfumo huu tumetengeneza kwa kuweka ‘controller’ ambazo zimepewa akili ambayo imepangiliwa na kompyuta kwa ajili ya kudhibiti mikonyezo ya macho.

Amesema dereva akisinzia atapata taarifa mara tano mfululizo na asiposikia mfumo utapunguza spidi hadi kufikia 20 kwa kuwa spidi hiyo si hatarishi na haiwezi kuleta madhara makubwa ikilinganishwa na anapokuwa kwenye mwendokasi.

Sauti hiyo itasikika hadi kwa abiria ikisema kuwa ‘dereva unasinzia kwa usalama wa abiria na watumiaji wengine wa barabara simamisha gari lako’ sauti ni kubwa hata abiria watasikia hivyo watajua dereva wao anasinzia, na sauti hiyo itaendelea mara kadhaa hivyo abiria kama watamrusu dereva kuendelea na safari wakati anasafiri wakipata ajali itkauwa ni uzembe wao.

Paschal amesema tayari wamepokea maombi ya uhitaji wa magari zaidi ya 1,000 ya kufungiwa mfumo huo.

Aidha, amesema wanatarajia kuweka  kifaa maalum kinachomzuia dereva kuendesha gari akiwa amelewa na tayari wameshaagiza vifaa hivyo vitakavyowasili hivi karibuni.

Habari Zifananazo

3 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button