Viashiria utapiamlo vyapungua Kagera

MKOA wa Kagera kwa kushirikiana na wadau wanahomasisha maswala ya lishe bora kwenye jamii umefanikiwa kupunguza viashiria vya utapiamulo na udumavu kwa watoto wadogo kutoka asilimia 41.7 hadi asilimia 34.

Afisa lishe mkoa huo, Johanitha Jovini alisema takwimu hizo zimefanyiwa utafiti na Demographics Health Survey ( DHS) kwa mwaka 2015 /2016 Khali ya lishe ilikuwa mbaya zaidi mkoani Kagera na mwaka 2022)2023 inaonyesha Jamii imeendelea kuonyesha uelewa mkubwa katika maswala ya lishe.

Alisema kuwa Sera ya maswala ya lishe imeendelea kutekelezwa na Serikali kwa kuendelea kutenga bajeti kwa watoto wa chini ya umri wa miaka 5 huku Mafunzo zaidi kwa wanawake wajawazito yakiongezewa nguvu tangu anapoanza kiliniki mpaka mtoto anapohitimisha miaka mitano huku wadau wa masuaala ya lishe Bora wakijitahidi kupenyeza Sera ya lishe kwa ngazi zote za chini,vyama vyote vya siasa mpaka kwenye utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi.

Kwa Niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Fatuma Mwasa Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Erasto Siima akifungua mafunzo ya awali ya mradi wa kuongeza upatikanaji wa chakula shuleni ambao unafathiliwa na Shirika la Harvest kupitia Agrithaman Kagera alisema swala la lishe bado linahitaji mkazo kwani mkoa unapaswa kubaki na asilimia zero ya lishe duni.

Alisema Sera ya lishe imefanikiwa kupenya na kuwalinda zaidi watoto walioko chini ya miaka mitano lakini kunamdororo mkubwa mkoani Kagera kwa watoto wa miaka 6 na kuendelea kwani wazazi wamekuwa wagumu kuchangia chakula shuleni hivyo watoto wanatumia muda mwingi shuleni bila kula chakula chochote.

Alisema kuwa mpaka Sasa ni asilimia 40 tu ya shule ambazo zinapata uji ama chakula shuleni mkoani Kagera huku watoto wengi wanaosoma wakikabiliwa na matatizo ya usikivu na afya mbovu kutokana na kutopata chochote kwa masaa 8 ya siku na kuwataka viongozi wajitafakari juu ya ushawishi walionao katika kuhakikisha wazazi wanakubari kuchangia uji na chakula shuleni.

“Napongeza wadau wa lishe kwa nguvu na nafasi Kubwa ambayo wametumia kuhakikisha wamama wanaonyongesha na wajawazito wanafata zile afua zote ,lakini kinachosikitisha hapa ni kuwa watoto wengi tuliowakoa chini wanaenda kudhoofika huku juu ,wazazi wa Kagera hawachangii uji, hakuna usikivu na watoto wanakumbwa na tatizo la kutoona kwa sababu ya njaa matokeo yake wanapata alama kidogo na mkoa unarudi nyuma tubadilike ili kuokoa kizazi chetu”alisema Siima.

Meneja wa Shirika la Agrithaman Mwasiti Kazinja alisema kuwa shirika hilo limefanya mabadiliko makubwa kwa kuhakikisha wanafunzi wanajifunza kuandaa bustani shuleni kwao na walimu wao hata kama eneo nifinyu kutoa elimu ya lishe ingawa Baada ya kuona mboga hazitoshi kuliwa na wanafunzi sasa shirika hilo limekuja na mradi wa kuongeza lishe kwa wanafunzi kupitia mahindi na viazi lishe vilivyoongezewa virutubisho.

Alisema mradi huo utanufaisha kata 9 Kati ya kata 14 za manispaa ya Bukoba ambapo wakulima,wanafunzi na waongeza thamani ya chakula wote watapata kunufaika na mradi huo kwa kupata mbegu za mahindi,kuandaa mashamba Darasa na jamii kujifunza faida za matumizi ya mahindi ,maharage na viazi vilivyoongezewa virutubisho katika jamii zao.

Mbunge wa viti maalumu kupitia mashirika yasiyo ya kiserikali na Mkurugenzi wa Shirika la Agrithaman Neema Rugangira alisema wadau wengi wa lishe wamepambana na maswala ya lishe kwa watoto chini ya miaka mitano hivyo nguvu hiyo kubwa kwa sasa itumike kwa watoto walioko shuleni ili kupunguza changamoto za lishe ambazo urithisha kizazi kimoja hadi kingine na kupelekea serikali kutumia bajeti kubwa kutibu maswala ya lishe duni.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button