Vibanda 12 vya biashara vyavunjwa Kigoma

VIBANDA 12 vya biashara vinavyojengwa katika eneo la Stendi Kuu ya mabasi mjini Kigoma vimevunjwa usiku na watu zaidi ya 20 wanaodaiwa walikuwa na silaha mbalimbali.

Hatua ya kuvunjwa vibanda hivyo inadaiwa kinatokana na kugombea mpaka baina ya mkandarasi aliyepewa tenda ya kujenga vibanda hivyo na mtu mmoja anayemiliki eneo jirani na vibanda hivyo, mali ya Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji.

Akizungumza na waandishi wa habari eneo la tukio, mzabuni aliyeshinda zabuni ya ujenzi wa vibanda hivyo, Ulimwengu Rashidi amdesema kuwa tukio hilo limetokea wiki hii ikiwa ni mara ya nne ndani ya kipindi cha mwaka mmoja, kufanyika kwa shambulio kama hilo.

Rashidi alisema kuwa vibanda vilivyovunjwa ni sehemu ya vibanda 22, ambavyo Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji imetoa zabuni vijengwe na kupangishwa, ili kuongeza mapato ya halmashauri hiyo na mzabuni huyo amedai kuwa uvunjaji huo umemtia hasara ya Sh milioni 75.

Ulimwengu Rashidi Mzabuni wa vibanda vya biashara vilivyovunjwa. Picha zote na Fadhil Abdallah.

Amedai kuwa ameshinda zabuni hiyo kihalali na kuanza ujenzi mwezi Februari mwaka jana, lakini hadi leo vibanda havijakamilika kwani kila akifika usawa wa kuweka paa uvunjaji unafanyika na kulazimika kubomoa, ili kurekebisha na hadi sasa kwa mara nne zote muhusika hajachukuliwa hatua zozote licha ya kujulikana na mamlaka husika.

Akizungumza kwenye baraza la madiwani la manispaa ya Kigoma Ujiji, Mkuu wa wilaya Kigoma, Salum Kali ametoa maagizo kwa kamati ya ujenzi ya manispaa hiyo kutembelea eneo, lakini kujiridhisha na umiliki wa eneo na mchakato wa kumpa zabuni mtu anayetekeleza mradi wa ujenzi wa vibanda hivyo, ili  taarifa hiyo  iweze kufanyiwa kazi.

Kali alisema kuwa mtu aliyefanya vitendo hivyo anapaswa kushughulikiwa kama mhalifu mwingine, hivyo ameomba taarifa hizo zifanyiwe kazi mapema kuwezesha hatua za kisheria kuchukuliwa hata kama mtu aliyefanya hivyo ana uhusiano na eneo hilo, lakini tukio lililofanyika ni uhalifu hivyo anapaswa kuadhibiwa.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Whitney Holland
Whitney Holland
29 days ago

Making extra salary every month from house more than $15,000 just by doing simple copy and paste like online job. I have received $18,000 from this easy home job. Everybody can now makes extra cash online easily.

By Just Follow………….. http://Www.Smartwork1.Com

Back to top button
1
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x