Vifo ajali ya Precision air vyafika 19, wamo marubani

Idadi ya vifo vya fikia 19

IDADI ya watu waliofariki katika ajali ya ndege ya Precision Air imefikia 19 wakiwemo marubani wa ndege hiyo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema na kuongeza kuwa serikali inaendelea kufanya uchunguzi wa ajali hiyo.

Majaliwa amesema baada ya hatua za uokozi kuokoa watu 26, ilitarajiwa kuwa idadi ya watu waliokuwa wamesalia kuwa 17 hata hivyo jitihada zimewezasha kuopoa miili 19 sawa na ongezeko la watu wawili katika idadi ya watu 43 waliokuwa kwenye ndege hiyo.

Majaliwa amesitisha shughuli za usafirishaji kupitia uwanja wa ndege wa Bukoba kuruhusu uchunguzi wa kina wa uwanja huo.

Advertisement

“Vifaa vya uokozi vya kisasa vilichelewa kufika lakini niwashukuru watu waliojitoa kusaidia katika juhudi za uokozi,” amesema Majaliwa.

Taarifa zimesema pia kuwa utambuzi wa miili ya marehemu utafanyika baadaye na serikali itatoa taarifa baadaye jioni ya Nov. 6