Vifo mafuriko Manyara vyafikia 23, majeruhi 30
MANYARA: Hanang: MIILI ya watu 23 imepatikana hadi alasiri ya leo Desemba 3, 2023 eneo la Katesh, Wilaya ya Hanang mkoani Manyara, ambalo limekumbwa na mafuriko kutokana na mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia leo.
–
Akizungumza muda mfupi baada ya kufanya ukaguzi wa athari za mafuriko hayo, Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga amesema waokoaji wamefanikiwa kupata miili 23 na majeruhi 30, ambapo majeruhi hao wamepelekwa Hospitali ya Tumaini Hanang na kati yao watano hali zao ni mbaya wamekimbizwa Hospitali ya Mkoa Manyara kwa matibabu zaidi.
–
“Uokoaji unaendelea, lakini pia jitihada za kutoa tope katika makazi ya watu, maeneo ya biashara na barabarani nazo zinaendelea,” amesema RC Sendiga.