Idadi ya waliofariki kutokana na tetemeko la ardhi nchini Uturuki na Syria imefikia 16,000. Ripoti ya Al-Jazeera inaeleza.
Vifo vimegawanyika sehemu mbili kubwa zaidi ikiwa Uturuki ambako wamefikia 12, 873 na 3,162 kwa Syria.
Mamlaka zinaeleza matumaini ya kupata manusura yanafifia na wakazi wa kusini mashariki mwa Uturuki na kaskazini magharibi mwa Syria wanakosoa juhudi za haraka za utafutaji na uokoaji.
Rais wa Uturuki, Recep Erdogan amekiri kuwa mamlaka za uokoaji zina mapungufu amesema “tuna mapungufu” katika majibu ya serikali yake alipotembelea baadhi ya maeneo yaliyoathirika zaidi kusini mwa Uturuki.
Zoezi la uokoaji linaendelea kwa maeneo yote mawili.