Vifuu vya nazi vyatumika kuchenjua madini

MTAFITI na Mbunifu wa Teknolojia ya kutengeneza Carbone ,Tiberius Mario amesema vifuu vya nazi vinakazi kubwa ikiwa ni pamoja na kutengeneza carbone inayotumika kuchenjulia madini na kusafisha maji.

Mario ameyasema hayo wakati wa semina ya waandishi wa habari iliyoandaliwa na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Jijini Dar Es Salaam.

Amesema ubunifu huo alioufanya unanafasi kubwa ya kudhibiti uchafunzi wa mazingira kupitia vifuu vya nazi na pia kuepusha magonjwa kama malaria na kipindupindu.

Advertisement

”Tunatengeneza Activated Cardbon kutoka katika vifuu vya nazi,Carbon ni vichembe vidogovidogo tunatengezea matundu ndani vinakuwa na corosty ndani hivyo vitundu vinatumika kukamatilisha dhahabu.

“Nimeegemea sana kwenye upande wa dhahabu na maji machafu ninabadilisha kifuu cha nazi kwenda kwenye Carbon ambayo kwenye migodi yote Tanzania hauwezi kupata dhahabu bila ya kuwa na Carbon ni Udongo baada ya kuchujwa lazima ipitishwe kwenye carbon dhahabu zitoke kwenye udongo,”amesisitiza.

Amesema hapa nchin hakuna kiwanda cha kutengeneza Carbon kwa asilimia 100 zinatoka nje ya nchi huku mikoa ya Pwani na Kusini kuna nazi nyingi zaidi ya tani 350000 kwa mwaka ambapo hutoa vifuu vingi.

Amebainisha kuwa ameona abadilishe na kuwa kitu chenye thamani kwa kutengeneza carbon.

“Nilifanya utafiti wakuzalisha kidogo sasa nazalisha za wasatani na nilishapeleka kwenye baadhi ya migodi pia katika viwanda vya maji inatumika kusafisha maji kwa kupinguza clorine katika maji ili yaweze kutumika na kuondoa harufu.

Mario amesema Kidunia wanaoongoza kwa zao la nazi ni Indonesia,India na Tanzania iko namba 16 ambao inazalisha nazi tani 382,164 kwa mwaka kiasi ambacho kinaweza kuzalisha vifuu vingi.

“Kama vifuu vilisipoangaliwa vizuri vinaweza kusababisha magonjwa mfano ukiacha vikanyeshewa na mvua mbu wake watakapokuu malaria yake ni kali pia uchafu unaokuwa katika kifuu cha nazi akitoa kipindupindu inaweza kutokea hivyo kubadilisha kunapunguza uchafuzi wa mazingira.

Amesema katika nchi kwa inaagiza nje Carbone zaidi ya tani 1500 kwahiyo inapoteza kiasi kingi ambazo ni dola milioni 6.7 .

“Mimi natumia kiwango kidogo ya vifuu 0.1 ya mimi ninachotumia nchini tunanunua nje wenzetu wanajua kutumia vifuu hiyo ninayotengeneza inaenda kuwasaidia wachimbaji wadogo wa madili kwani zinagharama nafuu na kuna wakati migodini zinaadimika mfano wakati wa corona,”ameeleza Mario.

Aidha amefafanua kuwa Carbone hiyo imeweza kupimwa katika maabara na utendaji wake ni asilimi 98 katika madini na maji asilimia 98 .

“Nilipeleka Mbeya,Sherui na Stamico na nilichukua sample nikapeleka tume ya madini matokeo yalitoka mazuri imekamata dhahabu kwa kiwango kikubwa
na pia ninaweza kurudisha tena kwenye system coarbone ambayo inatumika kwani carbone ikitumika haitakiwi kutupwa ila zinahifadhiwa hivyo ili kuondoa mrundikano narudisha.

Mario amesema Changamoto zinazomkabili ni mtaji wa kufanya uzalijishaji ambapo sasa anazalisha kilo 100 huku kiwango cha uhitaji kikiwa kikubwa .

Pia amesema chanzo cha joto anayotumia ni makaa ya mawe na kuni ambapo kitaalamu anahitaji joto zaidi ya 300,000 lakini kuni inanipa joto la 4000 kwa kilo moja ili kupata 300000 ninatumia kuni nyingi na muda ni mrefu.

“Nikipata disel burn joto lake ni kubwa ikilinganishwa na kuni na kifaa kinachotumika tutengeneza na kutoa bidhaa ninayotoa mimi ifike hata asilimia 90 sasa ni asilimi 50 nikiwezeshwa ninaweza kuchuku vifuu vyote na kutengeneza carbon hatutaagiza nje nahitaji Sh milioni 36,”ameeleza.

Amesema Carbone inuzwa mfuko mmoja wa kilo 25 Sh 250,000 hadi 400,000 inategemeana na nchi ambapo i China wanauza sh 250000 na 280000 na Amerika ni sh 400000 na kwa lakini rejareja kilo moja 20,000 hadi 25,000.

“Ni kitu cha gharama inaweza kuhitaji hata kilo 500 lakini uwezo wangu ni mdogo nikipata mtaji nitafanya vizuri,Pia sina nazi peke yake hata mchikichi naweza kutumi,”amesisitiza Mario.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *