CHAMA cha Wamiliki wa Kampuni za Ulinzi mkoani Arusha (TSIA), kinatarajia kuja na mpango kazi wa namna ya kufanya operesheni ya ulinzi kwa kushirikianana Jeshi la Polisi mkoani Arusha, lengo likiwa ni kudhibiti vitendo uhalifu.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa TSIA Arusha, James Rugangila na kueleza kuwa kesho chama chake kitakutana kuja na mpango kazi kwani wao ni sehemu ya walinzi muhimu katika nchi, hivyo ni wajibu wao kukutana kushirikiana na Polisi.
Rugangila ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Ulinzi ya Geo Securty ya jijini Arusha, alisema kuwa mgeni rasmi katika mkutano huo anatarajiwa kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Kamishina Msaidizi wa Polisi, Justine Masejo na utashirikisha wakurugenzi wote wa kampuni 69 za ulinzo mkoani hapa.