Trending

Vigogo Wizara, Bodi ya mikopo wahojiwa Dodoma

Mahojiano yadumu kwa takribani dakika 180

KAMATI ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii leo, Ijumaa, imewahoji viongozi wa Wizara ya Elimu na Teknolojia pamoja na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) jijini Dodoma.

Ikitumia takribani dakika 180 katika Ukumbi wa Pius Msekwa, Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti Stanslaus Nyongo iliwahoji viongozi hao kutii agizo la Spika Dk Tulia Ackson aliyetaka watendaji wa Bodi hiyo kuhojiwa kwanini hawataki kusikiliza maelekezo ya Serikali.

Waziri wa Elimu na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda akiambatana naibu wake, Omar Kipanga na Katibu Mkuu walikuwa wa kwanza kufika mbele ya Kamati hiyo.

Baada kuhojiwa viongozi hao wa Wizara kuhojiwa, walifuata Mwenyekiti wa Bodi ya HESLB, Profesa Hamisi Dihenga na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo, Abdul-Razaq Badru.

Baada ya zoezi hilo kukamilika majira ya saa 10 jioni, Mwenyekiti wa Kamati alisema mahojiano yalikuwa “mazuri” na kwamba taarifa hiyo itachakatwa na kuwasilishwa kwa Spika wa Bunge kabla ya kupata kibali cha kueleza ukweli utakaokuwa umebainika.

Habari Zifananazo

Back to top button