Vijana 295 wahitimu VETA Mwanza

VIJANA 295 kutoka Mwanza wamehitimu mafunzo ya ufundi katika fani mbalimbali Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) yaliyofanyika kwa miezi sita na kufadhiliwa na Benki ya KCB.

Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano wa benki hiyo, Christina Manyenye wakati wa hafla ya mahafali ya kuwapongeza wahitimu hao.

Manyenye amewapongeza wahitimu wote kwa kuweza kuhitimu masomo yao ya ufundi. Amesema benki yao imetoa ufadhili huo wa masomo kupitia mradi wa tujiajiri.

Amesema vijana mbal mbali wakitanzania wataendlea kusoma masomo ya ufundi na ujasiriamali kupitia mradi huo.

Amesema katika Mkoa wa Mwanza tokea mwaka 2016 ulipoanza mradi wa tujiajiri mpaka sasa vijana 625 wenye umri wa miaka 18-35 wameweza kunufaika na mafunzo ya ujasiriamali.

Amesema kupitia mradi huo katika mwaka 2019-2020 vijana 163 kutoka mkoa wa Dar-es-salaam walifanikiwa kujiunga na masomo VETA.

Amesema mpaka sasa kuna vijana 315 sehemu tofauti tofauti nchini wameweza kupata ajira baada ya kuhitimu mafunzo ya ujasiriamali yaliofadhiliwa na benki yao.

Mkuu wa Chuo cha VETA mkoa wa Mwanza Lupakisiyo Mapamba amesema wahitimu hao wa masomo ya ufundi walihitimu katika fani za upakaji rangi,Kuchomelea,Seremala na umeme wa majumbani.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x