ARUSHA: Vijana wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wameaswa kutumia kampuni ya biashara ya kuajiri ya Savanna ili wapate fursa za kupata kazi katika sekta mbalimbali zilizopo kwenye nchi ya Romania ili waweze kujikwamua kiuchumi
Ombi hilo limetolewa na Mwenyekiti wa Baraza la Biashara kutoka nchini Kenya,Stanley Kiplagat wakati wa uzinduzi wa ujio wa kampuni hiyo Jijini Arusha yenye lengo la kutoa fursa lukuki kwa watanzania katika kujikwamua kiuchumi wakiwa nchini Romania.
Amesema endapo vijana wakichangamkia fursa zilizopo nchini Romania watajikwamua kiuchumi sanjari na kuhudumia familia zao ambazo bado ni tegemezi hususan kwa nchi za Afrika sambamba na kubuni biashara pindi mikataba ya kazi inapoisha na kurudi nyumbani kwaajili ya kuwekeza zaidi
“Ukienda kufanya kazi huko, kesho utakuwa balozi mzuri sana kwa watanzania wengine, vijana msiogope kwenda ughaibuni fursa za kujikwamua kiuchumi zipo mzitumie ili mnaporudi mnawekeza nyumbani”
Naye Mkurugenzi wa Kampuni hiyo ya Savannah Recruitment Business Company nchini Tanzania,Tudor Nistor Alisema vijana wakitanzania na EAC kwa ujumla watumie fursa zilizopo nchini Romania kwaajili kujikwamua kiuchumi ikiwemo kuwekeza nyumbani kutokana na vipato watakavyopata
Amesema vijana wa Tanzania na wa EAC kwa ujumla wanatambulika zaidi kwa uchapakazi , ujuzi katika ufundi ikiwemo ubunifu haswa katika kilimo hivyo ni vema kutumia kampuni hiyo iliyosajiliwa nchini kwaajili ya kujipatia fursa lukuki za kufanya kazi katika nchi ya Romania
Comments are closed.