VIJANA waliopo katika mafunzo ya Kilimo chini ya Programu ya BBT katika kituo cha Mafunzo cha Bihawana-Dodoma wameishukuru serikali chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuja na program ya ‘Building A Better Tomorrow’ (BBT).
Kiongozi wa vijana Razack Mbaraka amesema mafunzo hayo yamekua na mchango mkubwa katika kuwaongezea maarifa juu ya kilimo Biashara na hivyo kuwaandaa kushiriki kikamilifu katika sekta ya kilimo.
Mbaraka ameyasema hayo wakati wa ziara ya Naibu waziri wa Kilimo , Anthony Mavunde alipotembelea kituo hicho na kujionea mafunzo yanayoendelea kwa vijana hao.
“Tunamshukuru Mh Rais Samia Suluhu Hassan na Wizara ya Kilimo chini ya uongozi wa Mh Hussein Bashe kwa fursa hii, mafunzo ya kilimo na kumilikishwa ardhi kwa vijana kupitia programu hii ya BBT imetuinua vijana.”Amesema
Naye Naibu Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde amewataka vijana hao kutumia fursa hiyo adhimu waliyoipata kwa kuchochea kuleta mageuzi kwenye sekta ya kilimo na kushawishi vijana wengi zaidi kushiriki.
Amesema, kundi hilo kubwa la vijana litoe mchango kwenye kukuza sekta ya kilimo nchini na kuahidi kwamba serikali itaendelea kuhakikisha inaboresha mafunzo haya ya vijana ili kuwaandaa vyema katika utelekezaji wa malengo ya Ajenda 10/30.
Akitoa maelezo ya awali Mratibu wa Programu ya BBT chini ya Wizara ya Kilimo *Bi. Vumilia Zinkankuba * amesema programu hii ya mafunzo inaendelea katika vituo 13 katika maeneo mbalimbali ya Tanzania na kwa sasa ipo hatua za mwisho na mafunzo hayo ya darasani na shambani na baada ya kukamilika kwake vijana watapelekwa mashambani kuanza uzalishaji wa mazao kwa vitendo.
Comments are closed.