Vijana kunufaika na umeme nuru

VIJANA  zaidi ya 200 katika mikoa minne nchini Tanzania wanatarajia kupewa mafunzo ya teknolojia ya umeme nuru (sola)kwa lengo la kuweza kujiajiri na kuajiriwa kwenye kampuni zinazotoa huduma ya  umeme huo kwa wananchi

Mikoa itakayonufaika na mafunzo hayo ni Simui,bShinyanga, Geita pamoja na Manyara kutoka Shirika la Kijerumani la GIZ kupitia  mradi wa ujuzi kwa maendeleo katika Afrika (E4D) kwa kushirikiana na chama cha nishati mbadala Tanzania (TAREA).

Akielezea kuhusu mradi huo Jijini Arusha, Katibu Mtendaji wa TAREA,Dk, Matthew Matimbwi amesema vijana  watanufaika na mradi huo kupitia katika halmashauri zao na watachaguliwa na wahusika kupitia kata zao ili wapate mafunzo ya umeme jua kwa lengo la kujiajiri wenyewe kama sera ya serikali inavyotaka kuwainua vijana kiuchumi.

Advertisement

Ametoa rai kwa wasichana kujitokeza kwa wingi katika mafunzo hayo ambayo darasani watafundishwa kwa wiki mbili kisha wataenda kwenye kampuni mbalimbali kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo na endapo wakifanya vizuri huko watakapopangiwa kwenye kampuni wanaweza kupata ajira moja kwa moja

Naye Msemaji wa GIZ, Faustine Msangira alisema  kuwa mradi huo wa E4D kwakushirikiana na TAREA wanautekeleza kwa lengo la kusaidia vijana hao wakiwemo asilimia 30 ya wanawake kupata ajira katika sekta ya nishati ya jua kama mafundi