Vijana Mbogwe watakiwa kumlinda na kumtetea Rais Samia
GEITA: Vijana wa Mbogwe mkoani Geita wametakiwa kuunga mkono jitihada za maendeleo zinazofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan ikiwa ni pamoja na kumtetea dhidi ya vikundi vya watu vinavyomkejeli na kumtukana.
Katibu Tawala wa Mbogwe Jacob Julius ‘ Jaju’ ameyasema hayo leo Mei 18, 2024 akizungumza na waendesha Bodaboda wilayani humo.
Jacob amesema Rais Samia ana imani kubwa na vijana ndio maana anaendelea kutoa fursa za kiuongozi kwa vijana, fursa za kiuchumi bila kujali itikadi za vyama vyao kwani kipaumbele cha Rais Samia ni utanzania kwanza.
“Takwimu za vijana waliojiajiri kwa kufanya kazi ya usafirishaji wilayani hapa ni zaidi ya 5,000, idadi hii ni ishara kuwa kazi ya bodaboda ni kazi kama kazi zingine,” amesema na kuongeza
“Hivyo inapaswa kuthaminiwa na fursa za mikopo zinazotolewa zisibague kundi hilo,”amesema.
Aidha, Jacob aliwaomba watumishi wa Benki zilizopo wilayani hapo kutoa elimu ya mikopo kwa wananchi.