‘Vijana ni nguzo muhimu maendeleo ya uchumi’

Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi

Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi, ameahidi kushirikiana na vijana katika  kufanya kazi za ujenzi wa maendeleo ya taifa kwa lengo la kuwainua kiuchumi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa matembezi ya vijana leo Januari 5, 2023 Zanzibar, Dk Mwinyi amesema vijana ni nguzo muhimu katika kusukuma maendeleo ya uchumi.

Matembezi hayo yaliyozinduliwa ni miongoni mwa shamrashamra za miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar ambayo kilele chake ni Januari 12 mwaka huu.

Advertisement

Pia Rais Mwinyi aliwasihi vijana kujiweka imara na kujitambua huku akisema wana nafasi kubwa ya kulitumikia taifa na kuliletea maendeleo.

“Shikamaneni na saidianeni, jitengezeeni ajira ili muweze kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili,” Dk Mwinyi alisema.

Pia alisema serikali imedhamiria kuwainua vijana kwa kuwapatia fursa za  ajira kwa namna iliyo bora na sahihi kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi.

“Serikali itawapatia mikopo itakayowaendeleza na tutazisimamia mamlaka husika, ili ziwape kipaumbele kwenye wepesi wa kupata hiyo,” aliongeza.

1 comments

Comments are closed.

/* */