Vijana shule ya polisi Moshi kuripoti kwa RPC Kilimanjaro

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Camillus Wambura amewatangazia vijana wa Shule ya Polisi Moshi kuripoti kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kilimanjaro na sio makao makuu ya jeshi hilo yaliyopo Dodoma kama walivyotangaziwa hapo awali.

Taarifa iliyotolewa leo na ofisi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi imeeleza kuwa vijana hao watatakiwa kuripoti April Mosi saa 12:00 asubuhi.

Vijana hao wametakiwa kutunza tiketi zao za mabasi watakayosafiria ili warudishiwe nauli zao watakapowasili Shule ya Polisi Moshi.

Aidha vijana waliofanya usaili Makao Makuu ya Polisi Zanzibar, na mikoa ya Tanzania Bara wata utaratibu utabakia kama walivyotangaziwa awali.

Habari Zifananazo

Back to top button