Vijana waathirika wakubwa Dawa za kulevya
Wazazi watakiwa kudumisha malezi bora
KUNDI la Vijana kuanzia miaka 15 hadi 35 limetajwa kuwa waathirika wakubwa wa dawa za kulevya.
Kufuatia hali hiyo, Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA) inatumia mbio za mwenge zilizozinduliwa mwishoni mwa wiki mkoani Mtwara na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kutoa elimu ya kutosha kwa jamii ili kuepuka matumizi ya dawa hizo.
Kamishna Jeneral wa DCEA, Aretas James Lyimo amesema kuwa mpaka sasa serikali imejipanga vizuri kuhakikisha udhibiti wa matumizi ya dawa za kulevya kwa vijana na hata jamii kwa ujumla yanafanikiwa nakupungua kabisa
Amesema, vijana kuanzia miaka 15 mpaka 35 ndilo kundi kubwa linaloathirika zaidi ambapo mpaka serikali imejitaidi kupambana japokuwa bado uuzaji wa dawa bado upo ijapokuwa unafanyika katika mazingira tofauti pia serikali inazidi kudhibiti njia hizo.
Nae, Kiongozi wa Mbio za Mwenge mwaka 2023 Abdalla Shaib Kaim amewasihi wazazi kudumisha malezi bora kwa watoto wao ili wasijiingize kwenye matumizi ya dawa za kulevya na kupoteza nguvu kazi ya Taifa.
Ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya ili kushirikiana kwa pamoja kumaliza tatizo la dawa za kulevya nchini.