Vijana wafundwa uboreshaji wa bidhaa

VIJANA wabunifu wameagizwa kutengeneza bidhaa zenye mahitaji sokoni ili kuwa na ubora zaidi utakaowawezesha kupata masoko na kujiajiri

Agizo hilo limetolewa katika eneo la Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) na Meneja wa Shirika la Viwanda Vidogo(Sido) ,Jafari Donge wakati wa kufunga mafunzo ya wiki ya ujasiriamali na ubunifu.

“Vijana tengenezeni bidhaa zenye mahitaji sokoni ili mpate masoko ndani na nje ya nchi lakini pia bunifu zenu ziwe zenye tija.

Naye mshindi wa kwanza wa shindano hilo,Prisca Anthony amesema ameonyesha bunifu maalum ya video inayoonyesha tafiti mbalimbali za vijana wa ndani na nje ya nchi kabla ya kuomba kazi au kubuni bunifu mbalimbali wanapaswa kufanya nini ili kuendeleza vipaji walivyonavyo.

Awali Mratibu wa Kituo Cha Ujasiriamali wa Chuo cha ATC,Donatha Mwase anasema vijana 24 walishiriki kuonesha bunifu zao na wabunifu watano sh,milioni 2.5 kila mmoja kwaaajili ya kuendeleza bunifu zao kutoka hatua ya wazo hadi katika kitu kinachoonekana na kusisitiza kuwa washindi hao watapata sh, milioni 12.5 ya kwaaajili ya motisha wa kuendeleza bunifu zao.

Habari Zifananazo

Back to top button