Vijana watakiwa kubadili tabia maambukizi VVU

Vijana watakiwa kubadili tabia maambukizi VVU

VIJANA nchini wametakiwa kubadili tabia katika pambano dhihi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi, ili kupunguza maambukizi baina yao.

Mkurungezi wa Takwimu, Ufuatiliaji na Utafiti wa Shirika lisilo la Kiserikali la MDH, Dk Lameck Machumi ametoa wito huo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu shughuli za shirika hilo kwenye mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi nchini.

Amesema kubadili tabia kwa vijana ni suala la kwanza katika mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi, huku akikisitiza umuhimu wa vijana kubadili tabia kupunguza maambukizi mapya baina yao.

Advertisement

Pia Dk Machumi ameshauri serikali na mashirika mengine kwenye mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi, kuweka mkazo katika suala la elimu kwa vijana kwa kutoa huduma rafiki ambayo itawawezesha kujiepusha na vitendo/tabia ambazo zinawaingiza kwenye hatari za kupata maambukizi ya VVU na Ukimwi.

“Tunaomba mashirika na serikali kuangalia sana katika eneo hili la kuelimisha vijana, lakini na kupeleka zile huduma rafiki kwa vijana,” amesema.

Meneja Mwandamizi wa Huduma za Tiba kutoka MDH, Dk Irene Andrew amesisitiza zaidi vijana wa kike kuhakikisha wanabadili tabia, lakini pia kujenga ujasiri wa kujiamini na kuwa na uwezo kusema hapana, pale inabobidi, ili kujikinga na maambuziki ya VVU.

Shirika la MDH linajishughulisha na utoaji wa afya kwa kushirikiana na serikali nchini kwenye maeneo ya mama na mtoto, maambuziki ya VVU, kufanya tafiti mbalimbali kusaidia muongozo ya serikali.

MDH inafanya inatekeleza kazi hizo kupitia ufadhili wa serikali ya Marekani chini ya mpango wa PEPFAR na CDC Tanzania.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *