Vijana watakiwa kuchangamkia fursa za kilimo

Vijana watakiwa kuchangamkia fursa za kilimo

VIJANA wametakiwa kuchangamkia fursa zilizopo kwenye sekta ya kilimo kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali mikubwa na programu za kuwawezesha,  ili kutatua changamoto kubwa ya ajira miongoni mwa vijana.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde  katika kongamano la vijana wa vyuo vikuu na vyuo vya kati lijulikanalo kama University Ladies and Gentlemen Conference, 2023, lililofanyika Kampasi ya Mazimbu-Chuo cha Kilimo Sokoine mkoani Morogoro jana Januari 28,2023.

“Serikali ya Tanzania chini ya Rais Dk  Samia Suluhu Hassan, kwenye kuhakikisha inachangia upatikanaji wa ajira kwa vijana, imetengeneza mazingira rahisi na kuondoa changamoto zinazowakabili vijana wanaojihusisha na kilimo kwa kuja na programu maalumu ya BBT yaani  Building a Better Tomorrow,” amesema.

Advertisement

 

Mavunde amesema kupitia programu hiyo ya  BBT, serikali inaenda kutatua changamoto zinazomkabili kijana kwenye shughuli za kilimo kwa kumuandalia ardhi iliyosajiliwa kwa ajili ya Kilimo, upatikanaji wa pembejeo, kupima afya ya udongo ili kufanya kilimo chenye tija, kumtafutia masoko, kumuandaa kwa mafunzo ya kufanya kilimo biashara katika kituo atamizi cha mafunzo ya Kilimo.

Awali Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu za kilimo (ASA), Dk Sophia Kashenge  aliwasistiza vijana kuitumia fursa hiyo iliyowekwa na serikali kufanya Kilimo na kueleza faida za kilimo na namna gani zinaweza kumpatia kipato Kijana.

3 comments

Comments are closed.