Vijana watakiwa kuchangamkia fursa za teknolojia

WAKATI dunia ikiendelea kufurahia kukua kwa teknolojia ya akili bandia, vijana wametakiwa kuchangamkia fursa hiyo, ambayo inasaidia katika kujiajiri.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa Kitengo cha biashara za simu za mkononi Tanzania, Mgope Kiwanga amesema mfumo wa akili bandia unamsaidia kijana katika kujiajiri kwa kufanya kitu ambacho mwanzo asingeweza kukifanya kutokana na ghalama za maisha.

Alisema teknolojia hiyo ambayo imekuwa msaada mkubwa sana katika nchi zilizoendelea imekuwa ikisaidia kujua maeneo au kitu ambacho kimefichwa kinapopatikana na kujulikana kinaweza kupatikana wapi hadi bei.

Advertisement

Alisema hii itasaidia sana kwa wapiga picha na watengenezaji filamu au kufanya utalii maeneo mbalimbali ya nchi kwa  kutambua eneo kwa kuangalia  picha iliyopigwa na mtu mwingine  ambapo teknolojia hiyo itaweza kumuonesha eneo hilo linapatikana wapi.

“Hii Teknolojia kwa sasa inapatikana hapa Tanzania kupitia simu ya Galaxy S24 Utra na Galaxy S24.

Ubunifu mkubwa wa teknolojia utaweza kurahisisha mambo mbalimbali, ikiwemo watumiaji kutumia lugha mbili tofauti na kuelewana na katika kufanya biashara” amesema.

Ameongezea kuwa teknolojia hiyo ya akili bandia kupitia simu ya Samsung, inaweza kumsaidia mtu katika kuandika barua katika ustadi nzuri iwe ya kuomba ajira au iwe ya kifamilia.