“Vijana wabadilishwe mitazamo kuziendea fursa”

RAIS Samia Suluhu Hassan amesema ni lazima vijana wabadilishwe mitizamo yao juu ya fursa mbalimbali zinazopatikana Afrika na kuondoa ile mitizamo ya kwenda nje ya bara hili kutafuta maisha.

Rais Samia ameyasema hayo leo Julai 26, 2023 katika mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika kuhusu rasilimali watu unaoendelea katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julias Nyerere Dar es Salaam.

“Idadi kubwa ya vijana tulio nao Afrikia ni fursa ya pekee kwa mageuzi ya uchumi wetu, kuliko kuwaacha wavuke bahari wapigwe njiani wazamishwe, kwa ajili ya kusema kwamba wanakwenda aulaya kutafuta maisha bora, maisha bora watayapata Afrika tukiwaendeleza,”amesema Samia

Advertisement

Aidha Rais Samia amesema ni lazima elimu ya uzazi itolewe kwa vijana ili kuendana na hali ya idadi ya watu ilivyo kwa sasa katika bara la Afrika.

“Ni lazima tuwafundishe watoto wetu kuhusu uzazi wa mpangilio, Afrika tuna idadi kubwa sana ya watu na hii inaweza kutuletea tija au kutuletea mambo yasiyofaa kama hatutoitumia vizuri,’amesema Samia.

Rais Samia ameongeza pia ni lazima kuongeza manufaa kutokana na elimu na mafunzo yanayotolewa katika nchi za Afrika ili kuongeza tija kwa vijana kukuza uchumi wa nchi za Afrika.

6 comments

Comments are closed.