Vijiji 30 kupatiwa ufumbuzi migongano binadamu, wanayamapori

WANANCHI waliopo katika vijiji 30 vilivyopo katika wilaya tatu za mikoa ya Lindi na Ruvuma watajengewa uwezo wa namna ya kupunguza migongano baina ya binadamu na wanyamapori.

Mchakato huo wa kuwajengea uwezo wananchi litaendeshwa na mradi wa Kupunguza Migongano baina ya Binadamu na Wanyamapori Tanzania, unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Ki jerumani-Tanzania (GIZ) kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii Tanzania.

Wilaya zitakazonufaika na mradi huo ni Namtumbo na Tunduru zilizopo mkoani Ruvuma na Wilaya ya Liwale iliyopo mkoani Lindi.

Mkuu wa Kitengo cha Mawalisiano Wizara ya Maliasili na Utalii, John Mapepele jana amewaambia waandishi wa habari za mazingira kuwa lengo la mradi huo ni kuwajengea uwezo watu wanaoishi karibu na maeneo ya hifadhi ili wawe na uwezo wa kudhibiti na kutatua changamoto hizo.

Akizungumzia mradi huo leo, wakati akifungua semina ya siku mbili iliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET), Mapepele amesema mradi huo utasaidia kupunguza kabisa migangano inayohusisha binadamu na wanyama pori.

“Wizara imepewa dhamana ya kusimamia na kulinda maeneo ya hifadhi ya Wanyamapori, Misitu na ustawi wa wananchi katika kukuza uchumi na ina mchango mkubwa kwa nchi kama chanzo cha mapato na ajira nyingi zinazalishwa.

Mapelele amesema uhai unategemea maji na viumbe hai na vyote viko kwenye maeneo ambayo yanalindwa ambapo misitu inatoa kivuli na nishati hivyo kama maeneo hayo hayalindwi yatapotea.

“Nchi inasifika kuwa na wanayama wanaotapakaa na kukuza utalii,kitoweo na mengi nguzo yetu nyingine ni kutangaza utalii wetu ambapo tunahitaji kuwekeza na ubunifu katika kutangaza rasilimali za vivutio vyetu.

Amesema wizara imeelekeza nguvu nyingi kutumia njia ya kisasa kutangaza utalii nje ya nchi ambapo sekta hiyo inachangia asilimia 25 ya uchumi na asilimia 21 ya fedha za kigeni.

“Nampongeza rais Samia kwani amekuwa mhifadhi namba moja kuhakikisha wanayama wanahifadhi kwa vizazi mradi huu lengo ni kuhakikisha wanahabari wanajengewa uwezo ili mwisho wa siku kujenga uhifadhi na kupata wataali wengi na taifa litaimarisha uchumi wake,”amesisitiza.

Mshauri kutoka Shirika la Maendeleo ya Ujerumani-Tanzania (GIZ),Anna Kimambo amesema lengo la kuchagua vijiji hivyo ni kutokana na kupata madhara makubwa yanayotokana na wanyamapori.

“Moja ya dhumuni ni kuhakikisha tunawajengea uwezo waandishi kuwa na mabadiliko ya uandishi kutoka hatua tuliyonayo kwenda hatua nyingine Mfano anaripoti tembo 200 wamevamia kijiji fulani kwa idadi ya tembo 200 hakuna mtu anapona lakini taarifa imetoka kwa mtu na tembo walikuwa wanapita tu habari hiyo inakuwa haitoi elimu.

Habari Zifananazo

Back to top button