VIKAO vya Kamati za Kudumu za Bunge vinatarajiwa kuanza Jumamosi Machi 11 hadi Machi 31, 2023 jijini Dodoma
Vikao hivyo vinatangulia kabla ya mkutano wa 11 wa bunge utakaoanza Aprili 4, 2023 ambao ni mahususi kwa mjadala wa bejeti ya serikali.
Taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Mawasilino na Uhusiano wa Kimataifa, ofisi ya Bunge mjini Dodoma, inasema kuwa shughuli zitakazotekelezwa na kamati pamoja na mambo mengine pia zitachambua mapendekezo ya mpango wa kiwango cha ukomo wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/2023
Pia, kamati hizo za kisekta zitatembelea na kukagua utekelezaji wa bajeti na kubainisha mambo muhimu yaliyojitokeza wakati wa kujadili utekelezaji wa miradi iliyotengewa fedha kwa mwaka wa fedha 2022/2023
Aidha, zitachambua taarifa za utekelezaji wa bajeti na kubainisha mambo muhimu yaliyojitokeza wakati wa kujadili utekelezaji wa bajeti za Wizara kwa mwaka wa fedha 2022/2023 na makadirio ya matumizi kwa mwaka wa fedha 2023/2024
“Kamati ya uwekezaji wa mtiaji ya Umma (PIC) itafanya ziara za kufuatilia utekelezaji wa miradi ya uwekezaji wa mitaji ya umma.” Imesema taarifa hiyo
Imesema, Kamati ya Hesabau za Serikali (PAC) itafanya ziara ya kutembelea na kukagua thamani ya fedha za umma zilizotumika katika miradi ya serikali kuu, mashirika na taasisi za umma.
Pia, Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) itafanya ziara za kufuatilia thamani ya fedha za umma zilizotumika katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo chini ya mamlaka za serikali za mitaa.
“Kamati ya sheria ndogo ndogo itapokea maelekezo ya ufafanuzi pamoja na kufanya uchambuzi wa sheria ndogo ndogo zilizowasilishwa bungeni wakati wa mkutano wa 10 wa Bunge.
“Vile vile kamati hii itapata mafunzo kuhusu uchambuzi wa miswada ya sheria na sheria ndogo.
Aidha, itapokea taarifa kutoka serikalini kuhusu utekelezaji wa maazimio ya Bunge yanayotokana na taarifa ya shughuli za kamati kwa mwaka 2022/2023
Wakati huo huo, kutakuwa na mkutano wa wabunge wote kwa ajili ya kupokea mapendekezo ya serikali ya mpango na kiwango cha ukomo wa bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2023/2024 kutoka wa Waziri wa Fedha na Mipango Mwigulu Nchemba umepangwa kufanyika Machi 13, 2023