Vilio vyatawala miili ya watoto waliofia mtoni

ARUSHA; HUZUNI na vilio vimetawala kwa wazazi, ndugu na jamaa, nje ya mochwari ya Kituo cha Afya cha Muriet kilichopo jijini Arusha, wakati miili ya watoto sita kati ya saba ilipofikishwa kituoni hapo.

Miili hiyo ilifikishwa muda mfupi uliopita na watu waliokuwa wakihangaika kuitafuta, ambapo vilio viliibuka kwa watu mbalimbali waliokuwepo kwenye kituo hicho.

Rahel ambaye ni mama mkubwa wa watoto Abigael Peter na Aboabol Peter waliofariki kwenye tukio hilo, amesema huo ni msiba mkubwa kwa familia.

Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Wilaya ya Arusha Mjini (UWT), Mary Kisaka ametoa pole kwa familia na kuongeza kuwa maelezo ya watoto walionusurika yanasikitisha, ni bora dereva angesubiri maji yapungue, ili apite.

Habari Zifananazo

Back to top button