Viongozi Afrika watakiwa kujitatmini

RAIS Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi wa Afrika kujitathmini na kuamua ni kwa namna gani wataweza kutumia uwezo na rasilimali za Afrika kujikwamua kiuchumi.

Ili kufikia malengo ya Ajenda ya kuitoa Afrika ilipo na kuifanya kuwa na uchumi imara kufikia 2063 ‘Transforming Afrika into the global power house of the future.’

Dk. Samia ameyasema hayo leo Julai 26, 2023 katika Mkutano wa Kimataifa wa Wakuu wa nchi za Afrika kuhusu ‘Rasilimali Watu’ katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa  Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam ambapo amesema ni muda muafaka sasa viongozi wa Afrika kulizungumzia hili kutokana na faida ya vijana barani Afrika.

Advertisement

Kiongozi huyo amenukuu takwimu za Jukwaa la Uchumi la dunia ‘World Economic Forum’

“Takwimu zinaeleza ifikapo 2050 Afrika itatoa nchi 10 zenye idadi kubwa za vijana duniani.” Amesema Samia na kuongeza

“Ifikapo 2030 Afrika itakuwa na asilimia 42 ya vijana wote duniani wenye umri chini ya miaka 25.”

Kiongozi huyo ameorodhesha mambo kadhaa ya kuzingatia ili kuwa na mageuzi ya kiuchumi kupitia rasilimali watu.

Mambo aliyoyataja ni pamoja na uzazi wa mpango, utoaji wa elimu bora, uimarishaji wa sekta ya afya na lishe kwa watoto pia kuwekeza katika sekta nyingine ikiwemo miundombinu ya usafirishaji, nishati, teknolojia na nyingine.

Aidha, katika hotuba yake ametaja changamoto zinazozirudisha nyumba nchi za bara la Afrika kufikia maendeleo

“Uhaba wa chakula, viwango vikubwa vya ukosefu wa ajira, umaskini uliokithiri na ukosefu wa usawa kwenye jamii.” Amesema Dk Samia

Itakumbukwa leo ni killer cha Mkutano huo unaotarajiwa kutoka na Azimio la pamoja kama bara kuhusu namna gani ya uwekezaji katika rasilimali watu itahakikisha ajenda ya 2063 inafikiwa.

Mkutano huo unadhaminiwa na Benki ya Dunia na unachagizwa kupitia mitandao  ya kijamii na ‘hashtag’ #InvestInPeople.

5 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *