VIONGOZI wa dini wamekemea vikali tabia ya baadhi ya viongozi wa dini kusimama katika majukwaa ya kisiasa kunadi vyama vya siasa kwa kufanya hivyo ni kugawa waumini na jamii.
Akizungumza kwa niaba ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) ,Padri Florence Lutaiwa amesema viongozi wa dini wana wajibu wa kukemea matendo maovu katika jamii na sio kupanda katika majukwaa ya kisiasa.
“Philosophy kuna mambo mawili ambayo mwanadamu anakutana nayo moja ni dini sisi viongozi wa dini tuna nafasi ya kusikilizwa ma tumeitwa ili viongozi wa dini tuweze kujua mipaka yetu katika siasa lengo letu sio kuchukua dola ila kuelekeza kufanya siasa nzuri mfano suala la bandari badala ya kujadilia kwa hoja sasa kinachoendelea dini imeingizwa.
Mwenyekiti wa Jumuiya na Taasisi za Kiisalamu Tanzania, Sheikh Musa Yusuph Kundecha ameeleza kuwa sio vizuri viongozi wa dini kuwa mshabiki wa chama fulani kwani viongozi wa dini kazi yao haitakiwi kuchanganya na siasa na dhambi ya siasa ni mbaya kwasababu inahusu watu wengi.
“Niseme kuwa siasa na dini ni changamani ni vigumu kutenganisha na siasa ni mambo ya jamii na viongozi wa dini wanajishughulisha ,asipande katika jukwaa la siasa kuonesha chama gani kinafaa waepuke ubaguzi na kubagua lakini alipaswa kukemea makosa ya kisiasa ni makubwa viongozi wa kidini wanatakiwa kuangali hili kwa umakini zaidi,”amesisitiza.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) Mchungaji Moses Matonyah amesema viongozi wa dini wanatakiwa kuwachunga Watanzania wote ambao wanatoka katika vyama vya siasa wote wanahitaji huduma kutoka kwao.
Comments are closed.