Viongozi wa dini waombea wanafunzi kidato cha sita
VIONGOZI mbalimbali kutoka madhehebu ya dini zote wamefanya maombi maalum ya kuombea wanafunzi wanaofanya mtihani wa kidato cha sita ,maombi ambayo yamefanyika uwanja wa shule za Kaizirege na Kemebosi mkoani Kagera .
Mchungaji Canon Elisha Bililiza kutoka kanisa la Anglican aliwaongoza viongozi wa dini na viongozi wa serikali walioongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Alberth Chalamila kuombea wanafunzi wote wanaofanya mtihani ya kidato cha sita na kujiepusha na vitendo viovu wakati baada ya kuhitimu masomo yao.
Wazazi walilazimika kushika vichwa vya watoto wao huku wachungaji mapadre ,mashekhe wakifanya maombi kila mmoja kwa zamu yake na kukemea vitendo vibaya ambavyo vinaongeza uvunjifu maaadili ya jamii ya Watanzania ikiwemo vitendo mapenzi ya jinsia moja.
Katika neno la utangilizi Bililiza aliwataka wazazi kutambua wajibu wao na kujua nafasi yao katika jamii hivyo wasione kulipa ada kama ndo jambo muhimu katika maisha ya watoto wao badala yake wanapaswa kuwafundisha watoto maadili, utii kwa Mungu,na umuhimu wakujitunza hasa wanapotaka kutumikia taifa lao.
“Mheshimiwa mkuu wa mkoa wa Kagera ,tunapongeza uwekezaji wa elimu uliofanyika hapa kemebosi kabla ya kuja Kama viongozi wa dini kufanya sala maalumu ya kuombea watoto tayari tulishakaa na watoto kwanza na kuongea nao lazima wajue dunia imebadilika lakini wao hawapaswi kufata mabadiliko mabaya hivyo mbele yako tunaomba wazazi pia watambue nini kinapaswa kufanyika “alisema Bililiza.
Mkuu wa mkoa wa Kagera Alberth Chalamila alisema kuwa mara Baada ya serikali kutangaza watoto wadodgo kutolewa katika shule za kulala tayari alituma timu ya uchunguzi kwa shule zote za bweni mkoani Kagera na shule za kemebosi na Kaizirege ndizo ziliibuka bora kwa kuwalea watoto kwa nidhamu na kuzingatia maadili yote yanayohitaji.
Hata hivyo kutokana na uwekezaji ambao umefanywa na mzaliwa wa mkoa wa Kagera na kufanya shule zake kutangaza mkoa wa Kagera kielimu kwa miaka yote 17 tangu kuanzishwa kwake aliwataka wakazi wa mkoa wa Kagera kufanya uwekezaji unaohakisi maendeleo kwa wanajamii wote kuliko kitu cha mmoja mmoja huku akiwahakikishia viongozi wa dini kuwa serikali inaendelea kusisitiza swala la maadili kwa watoto katika shule zote.
Mkuu wa shule za Kemebosi na Kaizirege, Kisha Ilamulila alisema kuwa ili kulinda maadili na vitendo vya ukatili mashuleni katika shule hiyo mfumo wa kamera umefungwa ndani na nje ya shule na wanafunzi ukutanishwa na viongozi wa dini mara kwa mara na kuongea nao juu ya kujifunza na kujiepusha na vitendo vinavyoweza kupelekea kutotimiza ndoto zao.
Shule ya Kemebos na Kaizirege imekuwa ikifanya vizuri kitaifa kwa mitihani ya kidato cha sita,nne,kidato cha Pili, darasala saba na darasa la nne tangu kuanzishwa mwaka 2007 ambapo mwaka 2023 wanafunzi wapatao 141 wanafanya mitihani ya kuhitimu kidato cha sita.