Viongozi wa dini waonya ushoga, usagaji

Viongozi wa dini waonya ushoga, usagaji

VIONGOZI wa dini Mkoa wa Arusha, wameonya jamii kuhusu suala la kuiga tamaduni za baadhi ya nchi za kimagharibi na kukemea vitendo vya mapenzi ya jinsia moja.

Pia wameomba serikali kumtazama mtoto wa kiume, ambaye amebaguliwa na kukandamizwa hali inayoleta athari hasi hata awapo shuleni hana ujasiri wa kutosha na kujieleza.

Akizungumza kwa niaba ya viongozi hao leo jijini Arusha, Askofu wa Kanisa la Anglikani Dayosisi ya Kilimanjaro na Mwenyekiti wa viongozi wa dini mkoani hapa, Stanley Hotay amesema masuala ya ushoga na usagaji na tamaduni nyingine za Kimagharibi haziruhusiwi Tanzania.

Advertisement

Viongozi hao pia walimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa uhuru wa vyombo vya habari na pia kuruhusu vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara.

 

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *