JUMUIYA ya Waislamu wa Ahmadiyya nchini imeipongeza serikali ya Tanzania kwa kuruhusu uhuru wa kuabudu na kuifanya nchi ya amani ambayo inasifiwa kuwa ni mfano wa kuingwa na mataifa mbalimbali duniani .
Sheikh Mkuu wa Jumuiya hiyo,Tahir Mahmood Chaudhry alitoa pongezi hizo mjini Morogoro wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 134 ya kuanzishwa kwa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya Duniani.
Alisema Tanzania ni nchi yenye amani na utulivu n ani ya kusifiwa kutokana na misingi yake imara ya Kurusu uhuru wa kuabudi na hivyo kupongezwa katika hilokwa sababu zipo nchi nyingine duniani hazina uhuru wa kuabudu.
Sheikh Mkuu wa Jumuiya hiyo alisema ,Jumuiya itaendelea kushirikiana na serikali katika masuala ya mbalimbali ya kusaidia utoaji wa huduma za kijamii kwenye sekta ya maji, afya na elimu.
“ Tunaunga mkono juhudi za serikali katika kusaidia utoaji wa husuma kwa jamii kama visima vya maji safi na salama , afya na elimu “ alisema Sheikh Mkuu wa Jumuiya hiyo.
Naye mkuu wa wilaya ya Kilosa, Shaka Hamdu Shaka akizungumza kwa niaba ya mkuu mkoa , Fatma Mwassa alisema, serikali inatambua mchango unaofanywa na taasisi za kidini mkoani humo na hapa nchini katika kuwahudumia wananchi.
Shaka alitolea mfano Jumuiya hiyo imekuwa ikichangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya nchi kwenye sekta mbalimbali ikiwemo elimu, afya, na maji kwa kuchimba visima katika maeneo mbalimbali ndani ya mkoa huo.
Mkuu wa Wilaya Shaka aliwahakikishia viongozi wa dini mkoani humo ya kwamba serikali itaendelea kuheshimu na kuthamini michango inayotolewa na taasisi za kidini ili kuongeza kasi ya kuwaletea wananchi maendeleo.
Mwakilishi wa Sheikh wa Mkoa wa Morogoro, Sheikh Saidi Kondo aliwashauri viongozi wa dini, serikali na wazazi kushirikiana ili kupambana na vitendo vya ukatili kwa watoto na masuala mengine maovu ndani ya jamii.
Sheikh Kondo alishauri elimu ya maadili mema iendelee kutolewa kwenye nyumba za ibada, kwenye familia na shuleni ili kuwakinga watoto kufanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia .
Kwa upande wake Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT), Dayosisi ya Morogoro, Jacob Ole Mameo, aliipongeza jumuiya ya waislamu wa Ahmadiyya kwa kuonesha ushirikiano mkubwa na madhehebu mengine ya dini nchini.
Askofu Mameo ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya Haki na Amani ya mkoa wa Morogorona alisema jumuiya hiyo ipo katika mstari wa mbele kutoa mafundisho yanayosaidia jamii zote bila kujadi dini zao.
Katika hafla ya maadhimisho hayo yalihudhuriwa pia na na wajumbe wa kamati ya haki na amani ya mkoa, kamati ya maridhiano ya mkoa na jumuiya ya waislamu wa bohora mkoani humo.