Viongozi wa kimila wamuombea Rais Samia

VIONGOZI wa Mila wa Jamii ya kifugaji ya  Kimasasi maarufu kwa jina la Laigwanani pamoja na viongozi wa dini wilayani Longido Mkoa wa Arusha,wamefanya maombi Maalumu ya Kumwombea Rais Samia Suluhu Hassan aendelee kuliongoza taifa hadi 2030 baada ya kufanikiwa kuifungua nchi kiuchumi.

Maombi hayo wameyafanya katika kijiji cha Mundarara kuhudhuliwa na idadi kubwa ya wakazi wa eneo hilo na vijiji vya jirani huku wananchi hao  wakiangua kilio na kuamsha Mori wakitaka Rais Samia apewe nafasi ya kuongoza taifa hadi 2030.

Kiongozi wa Malaigwanani Peter Sengeyon alisema maombi ya watu waliokusanyika hapo yamelenga kumshukuru Mwenyezi  Mungu kwa kumjalia afya njema Rais Samia na kumwomba Mungu aendelee kumlinda kiongozi huyo aweze kuongoza hadi mwaka 2030.

Alisema Rais Samia ameletwa na Mungu kwa makusudi ya kuisaidia nchi yetu hivyo lazima tumlinde na tumwombeee aishi na adumu kwenye uongozi wake hadi 2030

Naye Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Longido Papa Nakuta alimpongeza Mwekezaji wa Mgodi wa Ruby Bilionea Sendeu Laizer kwa kuwekeza mgodi huo ambao umekuwa msaada mkubwa na umenufaisha wa wananchi wa kijiji hicho pamoja na halmashauri ya Longido kwa kukusanya mapato ya serikali

Naye Mchungaji Daniel Kazimoto alisema maombi hayo yamfikie moja kwa moja Rais Samia  na kumpatia nguvu ya kusimama imara na kulitumikia Taifa Na kuwomba Mwenyezi Mungu kumjalia afya njema Rais Samia aweze kutawala hadi mwaka 2030.

“Watu wa Mundarara Mungu ametupa nyota inayong’ara tumwombee Rais wetu kila mtu kwa imani yake aombe hapa ili maombi haya yampe nguvu na moyo wa huruma Rais wetu Samia”

Habari Zifananazo

2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button