VIONGOZI na wadau mbalimbali wa Sekta ya Mawasiliano wakihudhuria Hafla ya Utiaji Saini Mikataba ya kupeleka huduma ya mawasiliano nchini inayofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma leo, Mei 13, 2023.
Mikataba hiyo inahusisha ujenzi wa Minara 758, katika mikoa 26, Wilaya 127, Kata 713 na Vijiji 1,407 vya Tanzania Bara.
Hadi kukamilika watanzania waishio vijijini wapatao 8,512,952 watapata huduma ya mawasiliano.