Viongozi wasiowajibika serikalini waonywa

Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo

VIONGOZI wa Serikali wasiowajibika ipasavyo, wamewashiwa taa nyekundu na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa hawatachekewa.

Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo ameyasema hayo leo Januari 24, 2022 mjini Dodoma katika mapokezi ya sekretarieti mpya ya chama hicho.

Amesema viongozi na watendaji wa serikali wanapaswa kuwajibika ipasavyo kwa wananchi na  kutekeleza ilani ya CCM badala ya kulalamika.

Advertisement

“Kuanzia sasa kiongozi asiyewajibika na kuishia kulalamika tu hatachekewa,” amesema.

Amesema baada ya sekretarieti mpya kuchaguliwa, kazi iliyopo ni kuhakikisha CCM inasimamia dola iliyopewa dhamana na wananchi kutekeleza yote yaliyoahidiwa na chama hicho, ili mwaka wa uchaguzi 2025 kusiwe na maswali mengi.

 

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *