Vishikwambi vya walimu kaa la moto

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimetoa wiki moja kwa Wizara ya Elimu kuanzia leo Januari 20, 2023, kuhakikisha vishikwambi vilivyotolewa na serika kwa ajili ya walimu vinawafikia walengwa.

CCM, imesema imepokea malalamiko ya kutotekelezwa kikamilifu kwa maelekezo ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuhusu ugawaji wa vishikwambi hivyo.

Akizungumza mjini Dar es Salaam leo, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Sophia Mjema, amesema wakati akizindua ugawaji wa vishikwambi hivyo Novemba mwaka jana, Waziri Mkuu Majaliwa aliagiza kuhakikisha vifaa hivyo vinakwenda kwa walimu.

Advertisement

Ulitengwa muda maalumu wa kutolewa kwa vishikwambi hivi ambao ulikuwa unaishia Januari 15, mwaka huu, lakini Chama kimepokea malalamiko kwamba hadi leo kuna baadhi ya makundi hayajapata hivyo vishikwambi. Lakini pia kuna baadhi ya wilaya hawajagawa kabisa vishikwambi hivyo.”Amesema Mjema na kuongeza

“Kuna maeneo mengine unakuta walimu wako 10 na wote wanahitaji na wanastahili kupata, lakini unakuta vishikwambi vinatoka vinane wawili wanaachwa.

“Chama kinatoa maelekezo, kinaielekeza wizara husika (Wizara ya Elimu) kuhakikisha zoezi hili linakamilika na walengwa wote wanaostahili kuhakikisha wameipata vishikwambi hivyo.”Amesisitiza

Aidha, amesema Wizara ya Elimu pia wahakikishe malalamiko hayo yanaisha na wasimamie zoezi kuona makundi yaliyopaswa kupewa yanafikiwa na wale ambao hawajapata wapate.

“Baada ya wiki moja tupate taarifa ya zoezi hili limekwendaje. “Amesema

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *